Golikipa mkongwe wa Misri Essam El Hadary amesaini kuichezea Wadi Degla kwa mkataba wa miezi sita kuanzia mwezi ujao.
El Hadary amemaliza mkataba wake wa kuichezea Al Merrikh ya Sudan mwezi uliopita.
Kipa huyo mkongwe amesema amesaini mkataba huo wa miezi sita ambao utafuatiwa na kusaini mkataba mwingine baada ya kumalizika miezi sita kama pande zote zitakubaliana.
Amesema alifanya mazungumzo na timu hiyo kuanzia mwezi uliopita na wamekubali kila kitu alichohitaji.
El Hadary anaongeza kuwa kumekuwa na ofa nyingi lakini ameichagua Degla kwasababu walihitaji sana huduma yake na amewaahidi kuwafanyia makubwa.
Inaelezwa kuwa TP Mazembe ya Congo DRC ilikuwa pia ikihitaji huduma ya kipa huyo lakini ameipiga chini ofa hiyo na kurejea kwenye ligi ya nyumbani Misri.
El Hadary amewahi kuzichezea timu za Al Ahly , Zamalek na Al Ismaily zote za Misri.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.