Friday, December 20, 2013
Ribery awalamba kisogo Algeria,kisa mapenzi ya mke wake
NYOTA wa Ufaransa anayecheza Bayern Munich Frank Ribery amedai kuwa timu ya Taifa ya Algeria itasonga mbele katika hatua ya makundi kombe la dunia licha ya kuwepo kwenye kundi H ambalo ni gumu.
Ribery mwenye miaka 30 amemuoa mwanamke wa kutoka Algeria Wahiba Belhami,na amekuwa akionesha kuizunga mkono timu za taifa za nchi hiyo za wadogo na ile ya wakubwa.
Anasema kama inavyofahamika mke wake ni raia wa Algeria na siku zote anamuunga mkono na ana furaha na watu wa nchi hiyo kwa timu yao kufuzu.
Algeria imepangwa na Russia, Belgium na South Korea katika kundi H,kundi linaloonekana kuwa gumu lakini Ribery anaamini timu hiyo iotafanya vizuri.
Anasema Algeria haitakiwi kujipa presha na kikubwa kucheza mchezo wao wa siku zote kwakuwa wanawachezaji ambao pia wanaviwangio vinavyostahili.
Algeria watafungua pazia kwa kucheza dhidi ya Belgium June 17 mwakani huko Estadio Mineirao mjini Belo Horizonte.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.