Louis van Gaal ametangazwa rasmi kuwa kocha mpya wa Manchester United, huku aliyekuwa kocha wa muda Ryan Giggs akitajwa kuwa msaidizi wake.
Raiya huyo wa Uholanzi, ametia saini mkataba wa miaka mitatu, na atachukua rasmi mikoba hiyo baada ya kuiongoza timu ya taifa ya Uholanzi katika fainali za kombe la dunia zitakazopigwa nchini Brazil.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 amewahi kushinda mataji na vilabu vya Ajax, Barcelona na Bayern Munich.
Manchester United ilimfuta kazi David Moyes mwezi Aprili, miezi 10 baada ya kurithi mikoba ya Alex Fergurson,aliyestaafu.
Gigs alikabidhiwa timu hiyo kama kocha wa muda katika mechi nne za mwisho za msimu uliopita na mkongwe huyo alikutana na Van Gaal nchini Uholanzi wiki iliyopita ili kuzungumza kuhusu hatima yake katika klabu hiyo, kama mmoja kati ya wakufunzi na wakati huo huo akiwa mchezaji.
Mchezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi Dirk Kuyt akimzungumzia kocha huyo amesema ni kocha mzuri,kocha wa ushindi na hata katika timu mbalimbali alizopita amepata mafanikio.
KUYT amesema kushinda mataji Uholanzi,Hispania na Ujerumani ni kitu kikubwa na ni kocha anayetaka mafanikio ikiwemo kwenye timu ya Taifa anayoinoa ambayo kwenye fainali za dunia 2010 nchini Africa Kusini walifika fainali wakachapwa na Hispania.
Mataji
Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96),
Barcelona (1997-98, 1998-99),
Bayern Munich (2009-10)Klabu bingwa ulaya:
Ajax (1994-95)Kombe la Uefa:
Ajax (1991-92)
Wakati akitajwa kama kocha msaidizi Giggs mwenye miaka 40 ametangaza
rasmi kutundika daruga zake akiwa ameweka rekodi ya kucheza mechi 963 huku
akicheza mechi 64 katika timu ya taifa ya wales.
Giggs ameshinda mataji 13,manne ya FA na mawili ya champions
league kati ya mataji 34 yaliyopo United.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.