Monday, May 5, 2014
Mourinho atangaza rasmi kusaka muuaji
Kocha Jose Mourinho amesema anataka kuongeza muuaji ambaye ataifanya Chelsea kuzichapa timu zote korofi msimu ujao.
Matumaini ya ubingwa kwa Chelsea yamepeperuka rasmi baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Norwich hapo jana.
Timu hiyo imekumbana na vichapo kadhaa msimu huu ikiwemo kutoka kwa Aston Villa, Crystal Palace na Sunderland katika siku za karibuni.
Amesema Chelsea inakosa mshambuliaji mwenye vitendo vya kutupia wavuni,kufungua geti na kupasia wavu.
Aidha akizungumzia mchezo wa jana Mourinho amewashutumu wachezaji wake kwa mchezo usio na kasi wala presha kwa wapinzani wao.
Mpaka sasa Manchester City wanaongoza kwa pointi 80 sawa na Liverpool iliyoko nafasi ya pili zikitofautiana kwa wingi wa magoli ya kufunga na kufungwa,Manchester City ina magoli 59 na Liverpool ina magoli 50 baada ya zote kucheza mechi 36.
Vinara hao wamebakiza mechi mbili mbili kukamilisha ligi kuu ya England msimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.