Kocha Hans Van de Pluijm ameibwaga Yanga baada ya mkataba wake kumalizika na tayari amepata kazi mpya huko Saudi Arabia.
Pluijm ambaye alishakubaliana na viongozi wa Yanga kama akipata timu nyingine ataondoka,alisaini mkataba wa miezi sita kuanzia mwanzoni mwa mzunguko wa pili,mkataba ambao umemalizika.
Sasa Yanga watalazimika kuingia kwenye mchakato wa kusaka kocha mpya au kumpatia mikoba kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa ambaye pia alipewa kazi ya kukinoa kigogo hicho mwanzoni mwa mzunguko wa pili akitokea Ruvu Shooting.
Kocha huyo ni kati ya makocha waliopewa sifa kubwa ya kuijenga Yanga katika siku chache alizokaa kwenye klabu hiyo na tayari amewasilisha ripoti yake ya wakati aliokuwa Yanga.
Pluijm anaondoka leo kwenda Saudia na hilo litakuwa pigo kubwa kwa Yanga ambao tayari wameanza kuvurugwa katika usajili baada ya mabingwa wapya wa Tanzania Azam FC kuwasajili wachezaji wake Didier Kavumbagu na Frank Domayo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.