Friday, May 16, 2014

Baada ya miaka 9 ya ukame wa mataji,Arsenal waanza kushangilia ubingwa wa FA,waandaa basi la kutembeza kombe


Arsenal hawajatwaa taji lolote kwa miaka tisa sasa lakini wanapewa nafasi kubwa ya kushinda taji la FA watakapocheza dhidi ya Hully City huko Wembley.

Kwa jeuri hiyo ya kuona tayari wana nafasi kubwa Arsenal tayari wameandaa basi watakalopanda wachezaji na kupita mitaa mbalilmbali ya huko London wakiwa na kikombe chao.

Tayari washika bunduki hao wameomba kibali cha kupitisha basi lao mitaani.

Picha imenaswa basi hilo likiwa limeshapambwa likiwa limeegeshwa sehemu likisubiri parade huku likiwa limepambwa na picha za ubingwa.

Parade hiyo itafanyika Jumapili ikiwa ni siku moja baada ya mchezo huo wa fainali.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.