Friday, May 16, 2014
KWELI UZEE MWISHO CHALINZE : Eto'o akataa uzee rasmi,amtusi kocha wake Mourinho
Kweli uzee mwisho Chalinze
Mshambuliaji wa Chelsea Samuel Eto'o amemtusi kocha wake Jose Mourinho akimuita mpumbavu kwa kuhoji kuhusu umri wake huku akitamba kuwa ataendelea kucheza katika soka la kiwango cha juu kwa miaka kadhaa ijayo.
Mourinho,ambaye pia alikuwa kocha wa Eto'o alipokuwa akiifundisha Inter Milan, alitia shaka umri wa Eto’o kuwa waweza kufika miaka 35.
Baada shaka hiyo Eto’o akamjibu Mourinho kwa kutumbukia wavuni na kushangilia kwa style ya kikongwe.
Mshambuliaji huyo amesema bado ataendelea kucheza soka la ushindani na ataendelea kucheza kwenye champions league baada ya kumaliza msimu akiwa kaifungia Chelsea mabao 12.
Akizungumzia kuhusu kombe la dunia Eto'o amesema wengi wanadhanai zitakuwa fainali zake za mwisho lakini kwake anaona bado anaweza kuendelea kucheza fainali zijazo atakapokuwa na miaka 37 kwakuwa wapo wengine walicheza fainali hizo wakiwa na miaka 42.
Mourinho baada ya mchezo wa mwisho wa ligi kuu dhidi ya Cardiff,alisema inawezekana Eto'o akaondoka katika klabu hiyo kwakuwa mkataba wake umemalizika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.