Timu mbalimbali zimeendelea kutangaza vikosi vyao kwaajili ya fainali za kombe la dunia 2014 zitakazopigwa nchini Brazil kuanzia June 12.
UHOLANZI
Robin van Persie ni mmoja wa wachezaji 7 wa ligi kuu ya England EPL waliotajwa kwenye kikosi cha Uholanzi kwaajili ya fainali za kombe la dunia.
Kocha Louis van Gaal ameita wachezaji 30 kabla ya kukipiga panga kikosi hicho ambacho kinamjumuisha Van Persie ambaye ameanza mechi moja akiwa na Manchester United baada ya kuumia mwezi March.
Beki wa Manchester City Karim Rekik,anayechezea kwa mkopo PSV Eindhoven naye kajumuishwa kwenye kikosi hicho.
WaDutch,hao ambao walipoteza kwenye fainali dhidi ya Hispania kwenye fainaali za 2010,wapo kundi B pamoja na Spain, Chile na Australia.
Wachezaji wengine wanaocheza EPL waliojumuishwa ni Michel Vorm na Jonathan de Guzman wanaocheza Swansea,golikipa wa Newcastle Tim Krul,beki wa Aston Villa Ron Vlaar na kiungo wa Norwich Leroy Fer.
Majina mengine ndani ya kikosi hicho ni pamoja na kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich Arjen Robben, kiungo wa Galatasaray Wesley Sneijder na mshambuliaji wa Fenerbahce Dirk Kuyt.
COLOMBIA
Colombia wamemtaja mshambuliaji aliyekuwa na hati hati ya kucheza fainali za kombe la dunia Radamel Falcao katika kikosi cha wachezaji 30 wakati huu akiendelea kufanya juhudi za kurejea uwanjani baada ya kuumia goti.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 anayechezea Monaco hajacheza tokea ameumia mwezi January lakini kajumuishwa kwenye kikosi na kocha Jose Pekerman.
Colombia wapo kundi C na Greece, Ivory Coast na Japan.
Colombia watafungua pazia dhidi ya Ugiriki June 14 huko Belo Horizonte,kabla ya kufuatiwa na mchezo dhidi ya Tembo wa Ivory Coast June 19 na kumaliza na Japan June 24.
Beki Pablo Armero,aliyecheza kwa mkopo katika mzunguko wa pili wa msimu katika timu ya West Ham United ni mchezaji pekee anayecheza England ambaye kajumuishwa kikosini.
ECUADOR
Nao Ecuador wamemjumuisha kikosini kiungo wa Manchester United Antonio.
Ndani ya kikosi hicho kocha Reinaldo Rueda amemjumuisha kiungo wa Stuttgart Carlos Gruezo, 19,ambaye amemuita kwa mara ya kwanza.
Pia kwenye kikosi hicho amewajumuisha wachezaji watatu wanaocheza nyumbani Cristian Penilla, Angel Mena na Armando Wila.
Ecuador wanahaha kusaka mshambuliaji wa kati tokea alipofariki Christian Benitez aliyekuwa anachezea Birmingham.
Timu hiyo ipo kundi E na Switzerland, France na Honduras.
URENO
Ureno nao wametangaza kikosi chake kilicho chini ya kocha Paulo Bento aliyemjumuisha kikosini nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.
Ronaldo amekuwa akisumbuliwa na misuli kwa takribani wiki nzima sasa huku akiukosa mchezo wa ligi ya Hispania ambao Real Madrid walichapwa mabao 2-0 na Celta Vigo.
Hata hivyo nyota huyo anatarajiwa atakuwa yuko sawa kwa mchezo wa fainali ya Champions league dhidi ya Atletico Madrid.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.