Wednesday, May 14, 2014
UCHAGUZI SIMBA : Zoezi la kuchukua,kurudisha fomu lafungwa
Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu kuwania uongozi wa klabu ya Simba linafungwa leo saa 10 jioni.
Fomu zinazotolewa ni katika nafasi ya Rais,Makamu wa Rais na wajumbe watano wa kamati ya utendaji.
Mpaka sasa nafasi inayozungumzwa kwa kiasi kikubwa ni ile ya Rais ambayo wagombea watatu wamechukua fomu Evans Aveva,Michael Wambura na Andrew Tupa.
Nafasi ya makamu wa Rais mpaka kufikia mchana ilikuwa na wagombea wanne wakiwemo viongozi wanaomaliza muda wao Swed Mkwabi na Joseph Itang’are Kinesi pamoja na Geofrey Nyange Kaburu.
Kwenye nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji wagombea 25 tayari wamejitokeza kuchukua na kurudisha fomu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.