Friday, August 23, 2013

Mata kwenda Man United?



Manchester United wametumbukia kumtaka kiungo mshambuliaji wa Chelsea Juan Mata ili atue Old Trafford kwenye usajili unaoendelea.

Hata hivyo haijawekwa wazi kama mpango huo ni sehemu ya sakata linaloendelea la mshambuliaji Wayne Rooney au kama United inataka kufanya makubaliano ya kubadilishana wachezaji hao.

Maneno ya Chelsea wakati huu wa usajili ni kwamba Mata hauzwi na inafahamika kuwa ni mmoja kati ya wachezaji watatu kipenzi cha mmiliki wa timu hiyo Roman Abramovich huko Stamford Bridge.

Hata hivyo inaonekana kwa Mourinho haoni hasara ya kuondoka kwa Mata na anafikiria zaidi kuimarisha sehemu yake ya ushambuliaji na ndio maana anamtaka Rooney huku tayari ikielezwa wametumbukia kumtaka mchezaji wa Anzhi Makhachkala Willian.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.