Friday, August 23, 2013

Tyson aonekana kutumia dawa za kuongeza nguvu



Mwanariadha wa Marekani Tyson Gay ameonekana kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni baada ya vipimo kuonesha hivyo.

Taarifa za mwanariadha huyo kuonekana kutumia dawa hizo zisizoruhusiwa michezoni zilitokea mwezi uliopita lakini haikuwekwa hadharani mpaka sasa.
Inaelezwa kuwa tayari wakala wa vipimo vya dawa zisizoruhusiwa michezo wa Marekani USADA wamemuandikia barua kumueleza kuhusiana na hilo.

Barua hiyo iliyoandikwa July 23 imeeleza kuhusiana na vipimo jinsi vinavyoonesha matumizi hayo ya dawa zisizoruhusiwa michezo.
Kwasasa inafahamika kuwa baada ya kuthibitishwa na wakala wa dunia WADA mwanariadha huyo atakumbana na adhabu.
Vinara wa kasi duniani kwa wanaume 100m
  • Usain Bolt (Jam) - 9.58 secs
  • Tyson Gay (USA) - 9.69 secs
  • Yohan Blake (Jam) - 9.69 secs
  • Asafa Powell (Jam) - 9.72 secs

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.