Monday, August 5, 2013

Tenga asema sasa uchaguzi wa TFF unanukia


Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Leodger Chila Tenga amezungumzia kupatikana kwa katiba mpya iliyopitishwa na kusajiliwa na msajili wa vyama na vilabu.

Tenga amesema kuwa kukamilika kwa hatua ya kwanza ya kupata katiba ya TFF, hatua inayofuata ni kuanza kwa mchakato wa zoezi la uchaguzi la kuwapata viongozi wapya watakaoiongoza TFF kwa kufuata kanuni na taratibu kwa mujibu wa katiba.
Aidha Tenga akawataka wadau kutoipindisha na kuitafsiri vibaya kauli ya naibu waziri wa habari,vijana ,utamaduni na michezo Amos Makala kwakuwa haikuwa na lengo la kupotosha ukweli juu ya usajili wa katiba ya TFF na badala yake alitaka kufahamu ukweli kuhusiana na uhalali wa usajili wa marekebisho ya katiba.

Kauli ya Makala ilikuja siku chache baada ya mkutano mkuu maalum wa shirikisho la soka Tanzania TFF uliofanyika July 13 mwaka huu, kufanya marekebisho ya katiba mpya ya TFF hatua ambayo Makala alisema haikuwa sahihi na marekebisho hayo yasingeweza kusajiliwa kwasababu hayakufata katiba ya TFF.

Ikumbukwe mapema mwaka huu Serikali kupitia wizara ya habari,vijana,utamaduni na michezo ilisimamisha zoezi la uchaguzi wa TFF kutokana na kutokuwepo katiba sahihi itakayouongoza uchaguzi huo, maamuzi hayo ya serikali yalipelekea shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFa kuionya kuifungia TFF endapo itabainika kuwa serikali inaingia utendaji wa TFF.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.