Makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Athuman Nyamlani amejitosa kuchukua na kurudisha fomu ya kuwania nafasi ya U Rais wa shirikisho hilo kwenye uchaguzi utakaofanyika October 27 mwaka huu.
Nyamlani amechukua fomu hapo jana kimya kimya bila ya makeke akitaka kuendelea kuutumikia mpira wa Tanzania.
Leo ndio mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu za kuwania uongozi kwenye nafasi mbalimbali za shirikisho hilo pamoja na zile za bodi ya ligi ambazo uchaguzi wake utafanyika October 18.
Kwenye nafasi hiyo ya Rais pia tayari Jamal Malinzi amechukua fomu za kuitaka nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.