Tuesday, August 20, 2013

Spurs bado inatamani kuingia sokoni


Kocha wa Spurs Andre Villas-Boas amekiri kusaka mchezaji mwingine kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili lakini akakataa kuongelea ripoti zinawahusisha na Willian wa Anzhi Makhachkala ya Russia.


 
Spurs tayari wametumia kitita kuwanasa Paulinho, Nacer Chadli, Etienne Capoue na mchezaji aliyesajiliwa kwa dau lililoweka rekodi kwenye klabu hiyo Roberto Soldado.

Matumizi hayo ya fedha yataendelea kama ambavyo Villas-Boas alivyobainisha kutaka kuongeza nguvu huko White Hart Lane.

Anasema wana kikosi kizuri na tayari wakiwa wameingia sokoni kuimarisha kikosi lakini bado wanatazama zaidi.

Akimzungumzia Gareth Bale,AVB anasema ni mchezaji ambaye yumo kwenye mipango yake licha ya kutakiwa na Real Madrid na jina lake limepelekwa kwaajili ya Europa league japo ni ngumu kumtumia Alhamis kwenye mchezo dhidi ya Dynamo Tbilisi kwasababu ni majeruhi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.