Monday, August 5, 2013

KIMENUKA MAN U : Rooney amwambia Moyes anataka kuondoka,United yakataa dau la pili la Chelsea

WAYNE ROONEY amengusha bomu baada ya kumwambia kocha David Moyes anataka kuondoka Manchester United na mazungumzo yao ya mdomo yatafuatiwa na maombi ya kutaka kuondoka kwa maandishi.


Moyes ana matumaini ya kuendelea kumbakisha Rooney Old Trafford lakini taarifa za uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa Rooney amemwambia uso kwa uso kuwa anataka kuondoka wakati wa mazungumzo ya wawili hao akimwambia sasa anataka kwenda kusaka chan gamoto mpya.

Rooney, 28 anataka kuungana na kocha wa Chelsea Jose Mourinho ambao wameongeza dau lao la kumtaka mchezaji huyo ambalo limekataliwa na United ambao wanasema hawawezi kumuuza mshambuliaji kama huyo kwenye timu nyingine ya Uingereza ambao ni mahasimu wao kwenye kuusaka ubingwa.
 

Rooney amemuhakikishia Moyes kuwa ataendelea kucheza kwenye klabu hiyo lakini moyo wake haupo tena kwa United kitu kinachomuumiza kichwa Moyes huku msimu ukibakiza wiki mbili kuanza.


Kocha wa zamani wa United Alex Ferguson aliwahi kuingia kwenye mzozo na mshambuliaji huyo baada ya kuomba kuondoka kwenye klabu hiyo

Jana usiku Chelsea walitumbukiza ofa ya paundi milioni 25 ili kuwashawishi United wamuachie Rooney,ikiwa ni ofa yao ya pili ambayo nayao imekataliwa na Manchester United wakisema Rooney hauzwi.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.