Tuesday, August 13, 2013

Baada ya kudai kuona jini ulingoni,bondia kuburuzwa mahakamani kwa udanganyifu

Kampuni ya masumbwi nchini TPBO imemtaka bondia Ramadhan Kido kurudisha fedha alizolipwa kwa pambano lake na bondia Chupaki Chipindi kutoka Iringa kwa madai ya udanganyifu ulingoni kwenye pambano lililofanyika Eid Mosi kwenye ukumbi wa Dar Live.

Rais wa TPBO LTD Yassin Abdallah Ustaadh kwenye taarifa yake amempa bondia huyo mwezi mmoja kurudisha fedha alizoplipwa kiasi cha shilingi laki 2 na akishindwa kufanya hivyo atamburuza mahakamani.

Hii ndio taarifa ya TPBO LTD,shuka nayo.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI -MICHEZO.NA WADAU.

NDUGU ZANGU WAPENDWA,

MARA NYINGI SANA TPBO-LTD TUMEKUWA TUKILAUMIWA SANA NA BAADHI YA WATU NA WADAU WA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA ,MARA TUNAPOKUWA TUKITOWA MAAMUZI MAGUMU YAHUSUYO MABONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA WANAPOVUNJA TARATIBU ZA MCHEZO HUU KWA MAKUSUDI.

ITAKUMBUKWA SANA MAAMUZI TULIYOWAHI KUYATOWA MWAKA JANA , KWA KUKATAA KUFANYA KAZI NA BONDIA MAARUFU SANA NCHINI FRANCIS CHEKA  KWA MUDA BAADA YA KUKATAA KWA MAKUSUDI KUPAMBANA NA BONDIA JAPHET KASEBA KATIKA TAMASHA LA MATUMAINI PALE UWANJA WA TAIFA.

WAKO BAADHI YA WANAOJIITA VIONGOZI WA NGUMI ZA KULIPWA WALIDIRIKI KUYAINGILIA MAAMUZI YA KAMPUNI YETUYA TPBO-LTD ILIYOSAJILIWA MAALUMU KABISA KWA AJILI YA KUSIMAMIA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA , NA KUYAPONDA KWA KUTETEA MAOVU YALIYOTOKEA ,NA HASA BAADA YA TPBO-LTD KUWAONDOLEA VIKWAZO MABONDIA KWA  KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA 2013 AKIWEMO FRANCIS CHEKA BADO WALIJITOKEZA BAADHI YAO HAWAKUTAKA  NIONDOWE VIKWAZO HIVYO KWA FRANCIS CHEKA KWA SABABU ZAO BINAFSI NA WALIJIONA WANAUMBUKA BAADA YA KUUDANGANYA UMMA WA WATANZANIA KWAMBA TPBO-LTD IMEMFUNGIA MILELE FRANCIS CHEKA,
 TAMASHA LA MATUMAINI LA MWAKA JANA LILIANDALIWA NA GLOBAL PUBLISHERS LTD.

SASA TAREHE 09-08-2013 KWA PAMBANO AMBALO LIMEANDALIWA PIA NA GLOBAL PUBLISHERS ,KAMPUNI YETU YA TPBO ILIPEWA MAJUKUMU YOTE YA KUSIMAMIA PIA KUWASAINISHA MABONDIA WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA MAPAMBANO YA NGUMI PALE DAR-LIVE SIKUKUU YA IDD-EL FITRI.

MIONGONI MWA MABONDIA WALIOSAINISHWA MIKATABA HIYO NI RAMADHANI KIDO ,NA MASHARTI YA MKATABA HUOKIFUNGU NAMBA 3 KINAELEZA WAZIWAZI KUWA BONDIA ATADAIWA PESA ALIZOZICHUKUWA KAMA MALIPO YA AWALI IWAPO ATAFANYA UDANGANYIFU KWA NIA YA KUKWEPA KUPIGANA ,NA HASA AKIJIANGUSHA ULINGONI BILA KUPIGWA NA HATA KAMA HAKUCHUKUWA MALIPO YA AWALI NA AMEJIANGUSHA KWA MAKUSUDI BILA HATA KUPIGWA NGUMI NA MPINZANI WAKE HATALIPWA MALIPO YOYOTE.
BONDIA RAMADHANI KIDO ALIPOPANDA ULINGONI KUPIGANA NA BONDIA CHUPAKI CHIPINDI ,KATIKA RAUNDI YA KWANZA TU DAKIKA MOJA TU NA SEKUNDE ISHIRINI ,WAKATI CHUPAKI CHIPINDI  ANARUSHA KONDE LA MKONO WA KULIA AMBALO HALIKUMPATA BONDIA HUYO ALIJIANGUSHA CHINI NA KUKATAA KUENDELEA NA PAMBANO.

KITENDO KILICHOSABABISHA WATAZAMAJI KUANZA KURUSHA CHUPA ZA MAJI KWA MAJAJI JAMBO AMBALO LINGESABABISA UVUNJIFU WA AMANI.

MIMI BINAFSI NILIPOMUHOJI KWA NINI AMECHUKUWA HATUA HIYO YA KUJIANGUSHA ,AKADAI MPINZANI WAKE ALIKUJA NA MAJINI ULINGONI ,JAMBO AMBALO LINAELEKEZA MOJA KWA MOJA ANAINGIZA MAMBO YA USHIRIKINA MICHEZONI ,JAMBO AMBALO TPBO-INALIPIGA VITA KWA NGUVU ZOTE.
Kushoto ndiye Chupaki aliyedaiwa na mpinzani wake kubeba jini ulingoni,kulia ni Francis Miyeyusho Chichi Mawe
HIVYO KWA MARA NYINGINE TENA TPBO-LTD INATOWA MAAMUZI MAGUMU KWA BONDIA RAMADHANI KIDO YA KUTOFANYA NAYE TENA KAZI ,MPAKA HAPO ATAKAPOJIREJEKEBISHA NA ILI KULINDA HADHI YA MCHEZO HUU TPBO-LTD HATUTAMUOGOPA BONDIA YEYOTE AMBAYE ATAJARIBU KUUFEDHEHESHA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA NA WALA HATUTAMUONEA AIBU KWA KUMUONDOWA KATIKA ORODHA YA MABONDIA WATAKAOTAMBULIWA NA TPBO-LTD.

ZIPO TAASISI ZINGINE ZA NGUMI ZA KULIPWA ANAWEZA KUSHIRIKIANA NAZO ,KAMA ZINARUHUSU VITENDO VYA KUWATAPELI WAPENZI AMBAO WANALIPA PESA ZAO ILI KUONA NGUMI ZIKIPIGWA BILA UBABAISHAJI.

TPBO-LTD ITAMPA BARUA RASMI KUPITIA KATIBU MKUU WAKE NDG IBRAHIMU KAMWE KUMJULISHA JUU YA MAAMUZI HAYA NA ATATAKIWA KURUDISHA TSHS 200,000 ALIZOCHUKUWA KWA TPBO  KAMA MALIPO YA AWALI,TPBO-LTD AMBAYO NDIYO ILIYOMSAINISHA MKATABA HUO

NA ATAPEWA MWEZI MMOJA ILI AWEZE KURUDISHA PESA HIZO ,NA KAMA HATARUDISHA NITAMSHTAKI KWENYE VYOMBO VYA DOLA KWA WIZI WA UDANGANYIFU

Imeletwa kwenu nami;-

Yassin abdallah Mwaipaya -Ustaadh
CHIEF PRESIDENT-TPBO-LIMITED [search google]
incorporated under companies ACT 2002 SECTION 15 REGISTRATION NO  95413

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.