Monday, August 26, 2013

Ancelotti asakamwa na mzimu wa Mourinho


Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amewataka mashabiki na waandishi wa habari kutojikita kutazama kipa gani atakayemchagua kusimama langoni kati ya Iker Casillas au Diego Lopez kwenye mchezo wa leo dhidi ya Granada.

Ancelotti aliwashangaza wengi alipoamua kumtumia Lopez kwenye mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Real Betis,wengi wakidhani Casillas angerejea golini baada ya kuondoka kwa Jose Mourinho.

Amesema klabu hiyo ina bahati kubwa ya kuwa na magolikipa wawili wazuri na anatakiwa kufanya chaguo ambayo ni jambo la kawaida kwake na hana sababu ya kusema atamuanzisha kipa yupi.

Kwasasa kuelekea mchezo huo Ancelloti anaumiza kichwa kwakuwa viungo wake watatu ni majetuhi,Xabi Alonso atakayekaa nje kwa miezi miwili mpaka mitatu , Sami Khedira na Asier Illarramendi.
 
Kiungo wa timu ya vijana Jose Rodriguez, 18,amesafiri na timu hiyo na inawezekana akawa kwenye benchi, Casemiro, 21,aliyenunuliwa kwa Euro milioni 6 akitokea Sao Paolo anaweza akapata nafasi ya kuanza.

Ancelotti anasema sehemu anayocheza Khedira,inaweza kuchezwa na Casemiro au Isco wakicheza karibu na Luka Modric.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.