Chelsea itakutana na Real Madrid Jumatano wiki hii kwenye fainali ya International Champions Cup baada ya kuichapa AC Milan 2-0 kwenye mchezo wao wa nusu fainali.
Magoli kutoka kwa Kevin De Bruyne na Andre Schurrle yalitosha kuwafanya Chelsea kuendeleza ubabe kwenye michezo ya kujiandaa na msimu mpya na sasa Chelsea wanajiandaa kucheza na timu ya zamani ya Jose Mourinho.
Mchezo huo umechezwa huko Miami kunako dimba la Sun Life
Mchezo huo wa fainali unatarajiwa kuwa na utamu wa aina yake kutokana na Mourinho kuwa kocha wa Madrid msimu uliopita kabla ya kurejea Chelsea na anakutana kwa mara ya kwanza dhidi ya timu yake ya zamani lakini raha zaidi atakuwa anatakutana kwa mara ya kwanza na kipa aliyekuwa akimuweka benchi Ike Casillas na Sergio Ramos.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.