Nyeti za kikao kilichoitishwa jana na Naibu waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Amos Makalla kujadili mkataba wa Azam Media kuonesha mechi za ligi kuu ambao umegomewa na Yanga zimevuja.
Supermariotz imenasa mambo yalivyokwenda ndani ya kikao hicho na kile kilichopitishwa.
Shuka nayo :
Yanga walikuwa na madai ama hoja nne kwenye kikao hicho :
Madai ya Yanga
1. Mgao wa pesa zaidi ya timu nyingine
2. Azam TV wanyimwe haki kwa kuwa wana timu ligi kuu
3. Kamati ya ligi haina mamlaka kisheria kwa hiyo mkataba uvunjwe
4.Mchakato(Tendaring) haikufanywa kwa uwazi kwa hiyo urudiwe tena
Kwenye kikao hicho mengi yalijadiliwa lakini hiki ndio ambacho kilipatikana baada ya majadiliano ya muda mrefu kutoka kwa wajumbe mbalimbali waliohudhuria wakiwemo viongozi wa Azam Media,viongozi wa Yanga,viongozi wa kamati ya ligi,viongozi kutoka wizarani,viongozi wa TFF na wajumbe kutoka vilabu vya ligi kuu.
MAJIBU
1. Mgao wa pesa zaidi ya timu nyingine haiwezekani na mgao unabaki palepale lakini Yanga wameshauriwa wakutane na Azam Media,na ikabainika kwenye kikao hicho kuwa ni kitu ambacho tayari kilichafanyika na walipewa ofa kama ya Simba lakini waliikataa lakini mbele ya kikao hicho wamelazimika kuikubali.
2. Hoja yao ya kutaka Azam TV wanyimwe haki kwa kuwa wana timu ligi kuu ambayo ni Azam FC imeshindikana na makubaliano ni kwamba Azam FC itaendelea kucheza ligi kuu na Azam Media wataonesha ligi kuu,na Kamati ya ligi imewaambia Yanga watoe mwanasheria ili ashiriki kwenye mkataba na imebainika kuwa ni hoja ambayo waliambiwa tokea zamani na vilabu vyote waliambiwa kama kuna mwenye mwanasheria wa mikataba kama hiyo ampeleke,Yanga hawakupeleka.
3. Hoja ya Kamati ya ligi kuwa haina mamlaka kisheria kwa hiyo mkataba uvunjwe imeonekana kuwa kamati ya ligi ina mamlaka kwahiyo hoja yao haina mashiko
4. Hoja ya kwamba mchakato(Tendaring) haikufanywa kwa uwazi kwa hiyo urudiwe tena imeonekana Yanga hawana hoja kwakuwa kila kitu kilikuwa wazi na SuperSport walishiriki wakashindwa na bado kuna uwazi mpaka sasa kwakuwa MoU(Memorandum of Understanding) ambayo wamesaini inaruhusu kama yupo mshindani mwenye hela zaidi ajitokeze na mpaka sasa hakuna mshindani aliyejitokeza wa kutoa fedha zaidi ya hizo zaidi ya bilioni 5.5 zitakazotolewa na Azam Media katika miaka yao mitatu ya mkataba.
Hayo ndiyo yaliyojiri kwenye kikao hicho,soma,tafakari na jibu utalipata.
Tatizo blogs ni hapo tu kuja na taarifa kabla ya wahusika kutoa halafu kwa ushabiki
ReplyDeletesupersport wanarusha mpira live south na bado wanamiliki timu iliyo ligi kuu south afrika vigezo walivyotumia vingine havina mashiko. Othewise na wao huyo ambaye anataka kuwadhamini asirushe mechi yoyote yao live awe anarusha mazoezi tu na vitu ambayo havihusishi timu nyingine.
ReplyDelete