Wednesday, August 14, 2013

SUAREZ : Siendi kokote nabaki Liverpool


Mshambiliaji Luis Suarez amekaririwa na gazeti la Uruguay la El Observador akithibitisha kuwa haendi kokote ataendelea kubaki Liverpool,na kuna ripoti kuwa anaweza kuongeza mkataba wa kuendelea kuwepo huko Anfield.

Uthibitisho huo ameutoa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uruguay iliyokuwa inajiandaa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Japan huko Sendai, Tokyo.

Suarez amesema kwasasa anachoweza kusema ni kuwaambia watu kuwa ataendelea kubaki kwenye timu hiyo.

Mapema leo mwandishi kutoka Latin America wa GolTV , Martin Charquero,amedai kuwa Suarez amemwambia kuwa hataondoka Liverpool licha ya Arsenal kuonesha nia ya kumuhitaji.

Mwandishi huyo ame tweet kwenye mtandao wa kijamii wa tweeter akisema kuwa Suarez amemthibitisha hataondoka Liverpool na mashabiki ndio wamepelekea maamuzi hayo aliyoyafanya.

Hiki ndicho alicho tweet Martin,kama unaelewa lugha hii twende sawa.

 “Luis Suárez me confirma que no se irá de Liverpool. El apoyo de los hinchas en las últimas semanas influyeron en la decisión”, escribió en su cuenta, antes de agregar que el salteño “ve como probable una renovación (extensión) del contrato que lo une a Liverpool”.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.