Crystal Palace wametangaza kuinasa saini ya mshambuliaji Marouane Chamakh kutoka Arsenal kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Chamakh, 29,alijiunga Arsenal akitokea Bordeaux kwa uhamisho huru mwaka 2010 lakini licha ya mwanzoni kuonesha makeke yake lakini baadaye akaporomoka kiwango chake na kuanza kulikalia benchi.
Mshambuliaji huyo raia wa Morocco msimu uliopita aliruhusiwa kwenda kwa mkopo kwa wagonga nyundo wa London West Ham Unitedna sasa ametimkia moja kwa moja huko Selhurst Park.
Tayari Palace imemnasa Kevin Phillips,aliyeongeza mkataba wa mwaka mmoja na Dwight Gayle,aliyesainiwa kutokea Peterborough.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.