Monday, August 12, 2013

Yaya aburuza tena Ivory Coast


Mwanasoka bora wa Africa Yaya Toure ametajwa kuwa mchezaji bora wa Ivory Coast 2012-2013 baada ya kushinda asilimia 32 ya kura zilizopigwa na waandishi wa habari za michezo na watumiaji wa Internet.

Kiungo huyo mwenye miaka 30 anayechezea Manchester City amefuatiwa na mshambuliaji Didier Drogba aliyepata asilimia 24 wakati mshambuliaji mpya wa Swansea Bony Wilfried akimaliza kwenye nafasi ya tatu akipata asilimi 17.

Arouna Kone, aliyejiunga Everton akitokea Wigan amepata asilimia15 wakati Gervinho naye amepata asilimia 15.

Toure ameshinda tuzo hiyo inayofahyamika kama Prix Sport-Ivoire kwa mara ya tatu baada ya kuhsinda mwaka 2008 na 2009.

Wakati huo huo Ivory Coast watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mexico Jumatano August 14 huko Metlife Stadium New Jersey, USA, huku Tembo hao wakiwa na nahodha wao Didier Drogba aliyerejeshwa kundini.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.