Friday, August 2, 2013

EXCLUSIVE : Manchester United yataka kuvunja benki kumrudisha Ronaldo

Manchester United na Real Madrid wametumia siku 12 kufanya makubaliano kuhusiana na mshambuliaji Christiano Ronaldo kurejea United ambako aliondoka kwa kwa dau linalokamata rekodi ya dunia la paundi milioni 80.

David Moyes aliamua kutumbukia kwa Ronaldo baada ya kusikia Madrid wanamtaka Gareth Bale huku ikielezwa Ronaldo mwenyewe yupo radhi kurudi England.

Mtendaji mpya wa United Ed Woodward amewasiliana na rais wa Madrid Florentino Perez kumuulizia Ronaldo ambaye mpaka sasa hajasaini mkataba mwingine wa kuendelea kubakia Bernabau na ule wa awali umebakisha miaka miwili kumalizika.
Perez alikuwa na uhakika wa Ronaldo kusaini mkataba mwingine wa kuendelea kubaki kwenye timu hiyo na taarifa kuwa yupo tayari kurudi England zimewashtua hilo pia limewafanya kukubali na United kuzungumzia mpango wa mchezaji huyo kurejea kwenye timu hiyo.
Real Madrid kutaka kutoa paundi milioni 85 kumnasa mshambuliaji wa Spurs na Wales Gareth Bale kunatajwa kuwa ni njia ya kuwapoza mashabiki wao kutokana na uwezekano wa Ronaldo kurudi zake United.
Kocha David Moyes tayari ameonesha nia ya kuhitaji huduma ya kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas kwa dau litakalovunja rekodi ya klabu hiyo ambayo kwa sasa inakamatwa na mshambuliaji Dimitar Berbatov aliposajiliwa kwa paundi milioni 30.75 akitokea Spurs.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.