Monday, August 12, 2013

Chelsea wafikiria kugeukia kwa Etoo kama watamkosa Rooney


CHELSEA wanafikiria kumnasa mshambuliaji wa Cameroon mkongwe Samuel Eto'o ikiwa kama mpango wa kumnasa Wayne Rooney hautafanikiwa.

Chelsea wanajiandaa kupeleka ofa ya tatu inayokadiriwa kufikia paundi milioni 28 na bado wana uhakika kuwa Rooney atakuwa mchezaji wao.



Lakini kocha Jose Mourinho katika saa 48 zilizopita ameonesha kumuhitaji Etoo anayecheza Anzhi Makhachkala kwa dau la paundi milioni 5.
Mourinho aliwahi kutaka kumasajili Eto’o,wakati alipokuwa akiifundisha Chelsea kwa mara ya kwanza lakini ikashindikana lakini akamfundisha wakati akiwa kocha wa Inter Milan,na kwasasa mshambuliaji huyo mwenye miaka 32 anapatikana kwakuwa klabu yake ina mkatatizo ya kifedha.

Eto’o alitua Anzhi akitokea Inter 2011 lakini wakali hao wa Russia wanalazimika kupunguza matumizi yao ya fedha kufikia nusu ya walichonacho na sasa wameamua kuuza wachezaji.

Inter na Napoli nao wanamtaka nyota huyo wa Cameroon.

 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.