Wednesday, August 14, 2013

Man City yangángána na Pepe


Manchester City wako tayari kupeleka ofa ya mwisho ya paundi milioni 20 ili kumnasa beki wa Real Madrid Pepe.

Bosi mpya wa Man City Manuel Pellegrini alikuwa anataka kununua beki wa kati kabla ya kuumia kwa Matija Nastasic katika wakati ambao kampeni mpya inaanza ya taji la ligi kuu England baada ya beki huyo kuumia kifundo cha mguu huku Pellegrini akishuhudia kikosi chake kikiruhusu goli nane kwenye mechi tatu za mwisho za kujiandaa na msimu mpya.


Pepe mara zote amekuwa chaguo la kwanza la Pellegrini lakini Real wamekataa ofa ya paundi milioni 15 mwezi uliopita na wamesisitiza kuwa wanataka aendelee kubakia huko Bernabeu. 

City wanataka kupeleka ofa nyingine inayofikia paundi milioni 20 kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa EPL wakicheza dhidi ya Newcastle.

Ripoti za Hispania zinasema Mkurugenzi wa michezo wa Man City Txiki Begiristain ameruka kwenda Madrid kujaribu kufanikisha mpango huo na kama wakichomolewa watazame upande mwingine.

Licha ya kutumia paundi milioni 90 kusajili wakati huu wa majira ya joto, City hawajasaini beki yeyote.

Baadhi ya mabeki wanaowanyemelea ni pamoja na beki wa Atletico Madrid Martin Demichelis na beki wa Schalke Kyriakos Papadopoulos huku pia wakihusishwa na beki wa Napoli Paolo Cannavaro.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.