Wednesday, August 21, 2013

EXCLUSIVE : Barthez aonesha daluga lilivyotaka kumchana mbavu

Golikipa namba moja wa Yanga Ally Mustapha Barthez ameonesha sehemu ya mbavu alipoumia kwenye mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam FC,maumivu yaliyompeleka nje baada ya kucheza kwa dakika zisizozidi 20 za kipindi cha kwanza.

Barthez anasema alijivika ushujaa kufuata miguuni mpira na kukutana na ajali hiyo iliyosababisha majeraha hayo.

Anasema kwasasa anaendelea vizuri na anafanya mazoezi mepesi mepesi kabla ya kurudi rasmi dimbani.
Sehemu ya mbavu aliyoumia Barthez

Kipa huyo ni mmoja wa wachezaji 24 walioitwa na kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Kim Paulsen ili kuivaa Gambia kwenye mchezo wa kuisaka tiketi ya fainali za kombe la dunia 2014 nchini Brazil.

Supermariotz tunakupa pole na kukutakia kila la kheri upone haraka.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.