Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Daring Club Motema Pembe ya Congo DRC ametua kwenye timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani Morogoro kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Mgosi amesema tayari wamemalizana kila kitu na Mtibwa na msimu ujao atakuwa na wakali hao wanaonolewa na kocha Meck Maxime.
Amesema ametazama mechi mbalimbali za Mtibwa walizocheza za kujiandaa na msimu anaamini kuwa atangára na klabu hiyo kwa mara nyingine na kuwatesa makipa wa timu pinzani.
Mgosi amewahi kuchezea kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kwa nyakati kadhaa,amewahi kucheza Simba alikosajiliwa kutoka kwa maafande wa JKT Ruvu na kabla ya kutua Mtibwa alicheza kwenye ligi kuu ya Congo DRC akiwa na DC Motema Pembe.
Hivi karibuni Mgosi alikuwa nchini China alikocheza mashindano maalumu ya mataifa ya Africa na kuibuka kuwa kinara wa kuzifumania nyavu kwa mara ya pili mfululizo kwenye michezo ambayo Tanzania iliibuka na ubingwa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.