Sunday, August 18, 2013

EPL : Mourinho akaribishwa na mabango Chelsea ikiwachapa Hull,Soldado aibeba Spurs

 
Mabao yaliyowekwa wavuni na Oscar Emboaboa na Frank Lampard yametosha kuipa Chelsea ushindi wake wa kwanza wa mabao 2-0 dhidi ya Hull City Tiger kwenye ligi kuu ya England mchezo uliopigwa Stamford Bridge.
 

Kwenye mchezo huo kocha Jose Mourinho amekaribishwa kwa mara nyingine na mashabiki wa klabu hiyo waliokuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.
 

Kabla ya mabao hayo Lampard alikosa penati iliyookolewa na kipa wa Hull City Tiger Allan McGregor,penati iliyotokana na kusukumwa kwa mshambuliaji Fernando Torres.
 
Katika mchezo mwingine bao lililofungwa na mchezaji ghali wa Spurs Roberto Soldado limeipa ushindi wa bao 1-0 Tottenham Hotspurs mbele ya Crystal Palace.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.