Thursday, August 1, 2013

Owino,Hamoud watiwa pingu Simba,Kaze naye atua

Wekundu wa Msimbazi Simba wamemalizana na beki wa kati raia wa Uganda Joseph Owino na kiungo MZanzibari Abdulghalim Hamoud.

Owino na Hamoud wote wamewahi kuitumikia Simba kabla ya wote pia kuitumikia Azam FC nayo ya Dar Es Salaam na sasa wamerejea tena huko Msimbazi ambapo leo wamesaini mkataba mbele ya kaimu makamu mwenyekiti Joseph Itangáre Kinesi,mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Said Pamba na mkurugenzi wa ufundi MGanda Moses Basena.

Owino amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia wekundu hao.
Hapa Owino anatia dole kwenye mkataba wa miaka miwili
Hapa Owino akikabidhiwa jezi ya kuitumikia Simba msimu ujao
 

Hamoud akisaini kuichezea Simba

Kinda Rahim naye akitia saini kuitumikia Simba
Wakati huohuo beki bora wa mashindano ya Kagame Gilbert Kaze kutoka Burundi anatua leo kumalizana na wekundu hao ambao wamedhamiria kujiimarisha kwaajili ya msimu ujao wa ligi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.