Tuesday, August 27, 2013

Mourinho ampa Rooney saa 48


Kocha Jose Mourinho amempa saa 48 mshambuliaji Wayne Rooney kuamua kama anaondoka au anabaki Manchester United au anatua Stamford Bridge.

Mourinho amemtaka Rooney kuomba kuondoka na aliweke suala hilo hadharani watu waelewe anachotaka.
United tayari wamesema mshambuliaji huyo hauzwi na alikuwemo kwenye kikosi kilicholazimishwa sare ya bila kufungana na Chelsea.

Mourinho tayari ametumbukiza ofa mbili ambazo zimechomolewa na Manchester United ili kumnasa nyota huyo ambaye katika mchezo wa jana alipokelewa vizuri na mashabiki wa klabu hiyo.
Alipoulizwa Mourinho kama atapeleka ofa ya tatu kama alivyoahidi kabla ya mchezo wa jana akasema Manchester United inaweza kuwa klabu ya kipekee,kwasababu klabu yoyote duniani ambayo mchezaji anataka kuhama hawawezi kumuunga mkono watampa wakati mgumu lakini imekuwa tofauti kwa United ambao wamemuunga mkono kwa asilimia zote kwenye mchezo wa jana.

Mourinho akasema amesema watakuwa wa kwanza kuheshimu kile atakachoamua Rooney.

Chelsea tayari wana chaguo lingine,ikielezwa kuwa rada zao zimemnasa mshambuliaji wa Anzhi Makhachkala MCameroon Samuel Eto'o na ndio maana wametoa saa 48 kwa Rooney ili wapate muda wa kusema na Etoo.
Wakati huo huo Rooney hana mpango wa kulazimisha kuondoka kwa kuwasilisha maombi ya kuondoka kimaandishi.
Licha ya mshambuliaji huyo kutotaka kulazimisha kuondoka inaelezwa bado mambo yake hayajapatiwa ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.