Wednesday, August 14, 2013

SAKATA LA AZAM TV : Yanga warudishwa kwa Azam Media


Yanga Africa wametakiwa kurudi kwa Azam Media kuhusiana na suala la kuongezwa dau kwenye mkataba wa kuoneshwa kwa mechi za ligi kuu.
Hii leo kumefanyika kikao kilichowakutanisha Yanga,Azam Media,TFF,kamati ya ligi na naibu Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Amos Makala.

Kwenye kikao hicho Rais wa TFF Leodger Tenga amezungumza wazi kuwa suala hilo la haki za kuonesha mpira ni la kikanuni na limekwenda kwa kufuata kanuni hivyo Yanga kama wanataka kuongezwa fedha hilo linabaki kati yao na Azam na si kamati ya ligi wala TFF.

Taarifa za kutoka ndani ya kikao hicho zimesema kuwa baada ya hoja za kila upande kujadiliwa,Yanga wameshauriwa kukaa na Azam na kuzungumza ili kufikia muafaka lakini haliwezi kubadilisha kuoneshwa kwa mechi za ligi kuu.

Yanga Africa hoja waliyokwenda nayo kwenye kikao hicho ya kuhoji uhalali wa mchakato huo imekosa nguvu kwakuwa imeonekana ni ya kwao binafsi na mchakato umefuatwa kama kawaida.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.