Programme mpya ya computer imetabiri kuwa kikosi cha Chelsea chini ya
kocha Jose Mourinho ndio watavikwa taji la ligi kuu ya England
itakapofika mwisho wa msimu.
Mahesabu hayo pia yanaonesha
kuwa Tottenham,wakiwa na Gareth Bale au wakiwa bila ya mshambuliaji huyo
watapambana kwa mara nyingine na Arsenal katika vita ya kuwania nafasi ya nne kucheza ligi ya
mabingwa Ulaya.
Programme hiyo ya Computer inaonesha kuwa
kutua Chelsea kwa Marco van Ginkel, Andre Schurrle na Mark Schwarzer
kutawabeba na kuwaimarisha watoto hao wa darajani kiasi cha kukaa juu ya mahasimu wa mji mmoja
Manchester United na Manchester City.
Timu ya Manchester City chini ya Manuel Pellegrini wanaonekana kuwa watamaliza nafasi ya pili juu ya mahasimu wao Manchester United.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.