Boss wa zamani wa the Toffees David Moyes ametoa ofa ya paundi milioni 16 kwa Fellaini,ambaye ana kipengele kwenye mkataba wake kinachomruhusu kuondoka kwa dau la paundi milioni 23 ambacho kimemalizika mwezi July.
United imetoa ofa ya paundi milioni 12 kwa Baines ambaye walijaribu kumsajili Mwezi June kwa dau hilo wakakataliwa.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Everton Alan Myers amethibitisha ofa hizo kuchomolewa akisema ni za kichekesho na tusi kwao.
Ofa hizo zilipelekwa mwishoni mwa wiki iliyopita na klabhu hiyo haikuliweka suala hilo hadharani kwakuwa kocha wao Roberto Martinez alikuwa kwenye maandalizi muhimu ya mchezo wa kwanza wa ligi.
Wachezaji hao wote wawili walikuwa kwenye kikosim cha kwanza kwenye mchezo ambao Everton walilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Norwich.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.