Wednesday, August 14, 2013
Manchester yamkata maini Mourinho,yasema Rooney hauzwi Chelsea kwa dau lolote
Mashetani Wekundu wa Manchester United wamekwenda mbali zaidi kwenye maamuzi yao wakisema mshambuliaji Wayne Rooney hatauzwa kwa bei yoyote kwenda Chelsea haijalishi kiasi gani cha fedha kitatolewa au ni madhara gani ya kuendelea kuwa na mtu asiye na furaha na klabu hiyo.
Maamuzi hayo yanamkata maini kocha wa Chelsea José Mourinho,ambaye aliweka bayana kuwa Rooney ndiye mshambuliaji chaguo lake na anahitaji huduma yake Stamford Bridge.
Chelsea tayari wamepeleka ofa mbili ambazo zimepigwa chini pundi milioni 23 iliyopelekwa July 16 na paundi milioni 25 iliyopelekwa August 4.
Maamuzi hayo ya United hayawezi kubadilika hata kama Rooney ataandika kwa maandishi maombi ya kutaka kuondoka.
Rooney ambaye amesema hana furaha kuendelea kubaki United,ameonekana na hali tofauti kwenye timu ya Taifa ya England inayojiandaa kucheza na Scotland leo usiku,akionekana ni mwenye furaha na akicheza na kufurahi na wachezaji wenzake.
United wanaamini kuwa Rooney atakubaliana na hali hiyo na atarejea kwenye hali yake ya kawaida ya kuwa na furaha ndani ya klabu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.