Cristiano Ronaldo amemuonesha mambo yake kocha wake wa zamani Jose Mourinho akipiga bao mbili wakati Real Madrid ikipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea usiku wa kuamkia leo kwenye Guinness International Champions Cup.
Ronaldo pia alitengeneza bao la kwanza lililotupiwa wavuni na Marcelo huku bao la Chelsea likiwekwa wavuni na Ramires.
Baada ya mchezo Mourinho amesema Ronaldo kufunga si habari lakini asipofunga ndio habari huku akimsifia kwa kiwango alichoonesha akisema ni mmoja wa washambuliaji wazuri.
Wakati Mourinho akicheza dhidi ya timu yake aliyoifundisha msimu uliopita,Real Madrid nao walikuwa chini ya kocha mpya ambaye aliwahi kuifundisha Chelsea 2009-10 akichukua taji la EPL na FA Carlo Ancelotti.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.