Tuesday, August 6, 2013

Chelsea bado ving'ang'anizi kwa Rooney,Ince naye atia petrol kwenye moto


Chelsea bado haijanyoosha mikono ya kumnasa mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney na wanajiandaa kupeleka ofa ya tatu.

Man U tayari wamekataa ofa mbili za Chelsea zilizotua kuhitaji huduma ya Rooney huko darajani.
 
Taarifa inasema kuwa Chelsea wanajiandaa kurudi tena kwa mara ya tatu wakiongeza dau la ,kumnasa mshambuliaji huyo ambaye hajatulia kwa mashetani wekundu wa Manchester United.

Tayari gwiji la zamani la Manchester United Paul Ince ametia petrol kwenye moto baada ya kusema kama Rooney kweli anataka kuondoka anatakiwa kulazimisha kuondoka kwenye klabu hiyo.
Ince ambaye kwasasa ni boss wa Blackpool amesema kama mshambuliaji huyo anataka kuondoka ni juu yake mwenyewe kulazimisha hilo litokee lakini mpaka sasa bado hajajitokeza kusema kama anaondoka au anabaki na itakuwa vizuri kujua nini mshambuliaji huyo anataka.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.