Miyeyusho amesema Lipupa anakuja kuchukua mkongóto ambao ataukumbuka kila anapokwenda kama ilivyokuwa kwenye pambano lake lililopita alilozichapa na bondia kutoka nchini Kenya ambaye alimkalisha mapema.
Bondia huyo anasema maandalizi yake yako sawa kwa pambano hilo alilowataka mashabiki wa Tanzania kujitokeza kwa wingi kwakuwa anabeba bendera ya nchi.
Miyeyusho akiwa na bondia kutoka Iringa Chupaki Chipindi |
Naye Rais wa kampuni ya masumbwi ya TPBO Yassin Abdallah Ustaadh amesema mabondia kutoka nchini Zambia wanatarajia kuingia nchini kesho saa 5 usiku tayari kwa mapambano hayo ya Eid Mosi.
Ustaadh amesema pia kutakuwa na pambano lingine kali kati ya Chupaki Chipindi kutoka Iringa akicheza na Ramadhan Kido wa dar Es Salaam.
Ustaadh na meneja mkuu wa Global Publishers Abdallah Mrisho |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.