Shirikisho la soka duniani FIFA limebariki maamuzi ya kuenguliwa kwa mshambuliaji wa zamani wa Inter Milan ya Italia na Monaco ya Ufaransa Mohamed Kallon kwenye nafasi ya Urais katika uchaguzi wa Chama cha soka cha Sierra Leone SLFA unaofanyika kesho Jumamosi.
Hiyo ina maana kuwa mwanamama Isha Johansen anabaki peke yake kwenye nafasi hiyo na akipata kura nitakazompitisha hiyo kesho atakuwa Rais wa kwanza mwanamke wa SLFA.
Maafisa wawili wa Fifa Primo Corvaro na Prosper Abega wametua Freetown jana Alhamis kufuatilia uchaguzi huo na walikuwa na kikao na Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma na kumwambia kuwa kamati ndio yenye uamuzi wa mwisho.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.