Luis Suarez amemaliza bifu lake na Liverpool na leo amefanya mazoezi baada ya kufanyika mazungumzo na kocha Brendan Rodgers.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 amerejea Merseyside jana kutokea kwenye timu ya Taifa ya Uruguay iliyocheza mchezo wa kirafiki na Japan na kuibugiza mabao 4-2 huko Miyagi.
Hata hivyo kilichozungumzwa kwenye kikao cha wawili hao kimeendelea kubaki siri yao japo kabla ya kikao hicho Rogers alisema atamruhusu Suarez kujiunga kikosini baada ya kuomba radhi kwa kile alichosema kuikosea heshima klabu hiyo.
Suarez alikuwa anatakiwa na Arsenal ambao waliwasilisha ofa mbili ambazo zilipigwa chini japo taarifa zinasema kuwa hawajakata tamaa na wanataka kuwasilisha dau la mwisho la paundi milioni 49.
Wakati ligi ikitarajia kuanza kesho,Suarez atakaa nje ya dimba kwa mechi sita za kwanza akiendelea kutumikia adhabu ya kufunguiwa mechi 10 kwa kumngáta beki wa Chelsea Branislav Ivanovic.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.