Robert Lewandowski ameushambulia uongozi wa klabu yake ya Borussia Dortmund akisema ametendewa sivyo kuhusiana na matakwa yake ya kutaka kujiunga na Bayern Munich.
Makubaliano ya mshambuliaji huyo kutua Bayern Munich yameshindikana kwa Dortmund kumtaka amalize mkataba wake uliosalia mwaka mmoja na ataondoka bure.
Lewandowski alikuwemo kwenye kikosi cha Dortmund kilichoichapa maba0 4-2 Bayern kwenye German Super Cup.
Ilionekana ni kama masuala yake ya usajili wa kuhamia Bayern sasa yamefungwa rasmi lakini Lewandowski,ambaye alifunga mabao manne dhidi ya Real Madrid kwenye nusu fainali ya champions League msimu uliopita amelianzisha upya na anasema anahisi amesalitiwa na Dortmund.
Lewandowski anadai kuwa aliahidiwa Euro milioni 6 na bonasi kama atabaki kuelekea mwisho wa mkataba wake lakini jambo ambalo halijatekelezeka.
Mshambuliaji huyo alitua Dortmund akitokea Lech Poznan ya Poland mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.