Wednesday, September 11, 2013

Zidane apewa kazi ya kumbakisha Casillas Madrid

Gwiji la Real Madrid Zinedine Zidane amepewa kazi ya kuhakikisha golikipa Iker Casillas haondoki kwenye timu hiyo.

Casillas, 32,tayari amezivutia klabu za England Manchester City na Arsenal  baada ya kukosa namba huko Bernabeu.

Lakini Zidane,anayefanya kazi ya ubalozi wa klabu hiyo amesema haamini kama Casillas ataondoka kwenye klabu hiyo lakini ni bora kuwa na mazungumzo naye ya uso kwa uso.


Casillas ameipoteza nafasi yake ya kusimama langoni kama kipa namba moja wa klabu hiyo tokea enzi za kocha Jose Mourinho aliyeamua kumuamini golikipa Diego Lopez.

Naye kocha mpya Carlo Ancelotti hajamrudisha Casillas kama namba moja tokea ameichukua timu hiyo hilo likimfanya kipa huyo kufikiria kuondoka.


Manchester City,inayofundishwa na bosi wa zamani wa Real Madrid Manuel Pellegrini,wanafuatilia kwa karibu hatima ya kipa huyo na kama inawezekana akapatikana kwenye usajili wa dirisha dogo mwezi January.

Barcelona pia wanaelezewa kufuatilia kwa karibu lakini inaonekana kuwa kuna ugumu kwa wao kuweza kumchukua kipa huyo.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.