Friday, September 13, 2013

ETOÓ : Nilimchukia Mourinho



Mshambuliaji mpya wa Chelsea MCameroon Samuel Eto'o anasema ukaribu wake na kocha Jose Mourinho ulianzia kwa waili hao kuchukiana.

Etoo mwenye miaka 32 anasema Mourinho ndio chachu ya yeye kujiunga na Chelsea baada ya kuonja matunda yake walipotwaa taji la Champions League 2010 wakiwa na Inter Milan.
 
Anasema mwanzoni kabla ya kufanya kazi pamoja kila mmoja alikuwa anamchukia mwenzake lakini walipofanya kazi pamoja ndipo ukaribu wao na urafiki ulipotokea.

Eto'o amesaini Chelsea mkataba wa mwaka mmoja akitokea Anzhi Makhachkala ya Russia kwa uhamisho wa bure.
Mwanasoka bora wa Africa mara nne alikuwa mchezaji anayelipwa zaidi dunia baada ya kutua Anzhi in 2011,lakini akaakutana na kadhia ya kukatwa mshahara wake kwa paundi milioni kutokea kupata paundi milioni 17 mpaka paundi milioni 7 wakati Anzhi wakikumbwa na kuyumba kwa uchumi wako kulikomfanya atimkie Stamford Bridge.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kitabu kinachozungumzia maisha yake Eto'o anasema alipenda kwa mara nyingine kufanya kazi na Mourinho.
Rekodi za Etoo kwenye klabu


Real Mallorca (1999-2004): Copa del Rey (2003). Scored 69 goals in 165 appearances.
Barcelona (2004-2009): Champions League (2006, 2009); La Liga (2005, 2006, 2009); Copa del Rey (2009); Spanish Super Cup (2006, 2007). Scored 129 goals in 201 appearances.
Inter Milan (2009-2011): Champions League (2010); Serie A (2009); Coppa Italia (2010, 2011), Italian Super Cup (2010); Fifa World Club Cup (2010). Scored 53 goals in 101 appearances.
Anzhi Makhachkala (2011-2013): Scored 36 goals in 71 appearances.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.