Tuesday, September 17, 2013

JONJO SHAVLVEY aomba radhi kwa kuibeba Liverpool


KIUNGO wa Swansea Jonjo Shelvey amewaomba radhi mashabiki wa Swansea kwa kufanya makosa yaliyofanya wapate sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo wa ligi kuu ya England EPL dhidi ya timu yake ya zamani Liverpool uliopigwa jana usiku huko Liberty Stadium.

Shelvey aliifungia Swansea bao la kuongoza kabla ya pasi yake ya nyuma kumpa nafasi Daniel Sturridge kusawazisha.
 

Victor Moses akaifungia Liverpool bao la pili kufuatia tena makosa ya Shelvey,lakini yeye mwenyewe tena akahusika kwenye bao la kusawazisha baada ya kumtengenezea pasi Michu na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao hayo 2-2 ambayo yote yamemuhusisha Shalvey.
 

Shelvey ameomba radhi kwa mashabiki kwa makosa mawili mabaya aliyoyafanya yaliyowapa Liverpool mabao hayo mawili.

Mchezaji huyo anayechezea kikosi cha vijana chini ya miaka 21 cha England alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Liverpool tokea alipoondoka Anfield kwa dau la paundi milioni 5.

Makocha wote wa Swansea Michael Laudrup na wa Liverpool Brendan Rodgers wako nyuma ya mchezaji huyo wakiamini ndio mwanzo wa kupata uzoefu zaidi.

Laudrup anasema wakati wa mapumziko aliongea naye na kumwambia bado kuna dakika 45 nyingine na hana sababu ya kukata tamaa kitu ambacho alikionesha.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.