Kinda raia wa Brazil aliyetua Chelsea huku Spurs wakiamini ni mchezaji wao Willian yuko tayari kuisaka namba kwenye kikosi hicho japo anaamini atakumbana na wakati mgumu matumaini yake yanabaki kwa kocha Jose Mourinho ambaye anasema kama atamuamini na mashabiki wakamuamini watayaona majibu yake.
The Blues wamekamilisha usajili wa kinda huyo kutokea Anzhi Makhachkala ya Russia kwa dau la paundi milioni 25.5 mwishoni mwa mwezi uliopita akisaini mkataba wa miaka mitano na amekabidhiwa jezi namba 22.
Willian anakumbana na upinzani kutoka kwa Eden Hazard, Oscar, Juan Mata, Ramires, Andre Schurrle na Kevin De Bruyne miongoni mwa majina yanayowania kuanza kikosi cha kwanza.
Lakini mwenyewe anasema anafahamu changamoto inayomkabili lakini atafanya kwa uwezo wake wote kuipata nafasi hiyo na kumshawishi kocha.
Willian anaamini kutua kwake Chelsea kunaongeza nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil kwaajili ya michuano ya kombe la dunia mwakani.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.