Mcheza Tennis raia wa Croatia Marin Cilic amefungiwa miezi tisa baada ya kupimwa na kuonekana kutumia dawa za kuongeza nguvu aina ya nikethamide.
Vipimo hivyo vilibanisha kuwa anatumia dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku michezo baada ya kuchukuliwa haja ndogo huko Munich mwezi April.
Cilic mwenye miaka 24 hajaonekana kwenye mashindano yoyote tokea alipojiondoa kwenye michuano ya Wimbledon,na amesema atakata rufaa kupinga mamuzi hayo kwa mahakama ya usuluhishi ya michezo.
Adhabu hiyo imerudishwa nyuma ikionekana kwamba inaanza kutumika May Mosi na kumalizika February Mosi.
Cilic,anasema mmoja wa watu wake kwenye timu alikwenda kwenye duka la dawa na kumnunulia dawa hizo ambazo kama Glucose.
Anasema hajadili kuhusu kesi hiyo lakini anashangaa Gluocose hiyo inafungiwa kutumika kwa wanamichezo kwenye mashindano lakini nje ya mashindano inaruhusiwa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.