Tuesday, September 17, 2013

Ripoti ya mwamuzi yainyonga Yanga



Ripoti ya mwamuzi wa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara kati ya wenyeji Mbeya City dhidi ya mabingwa watetezi Yanga Africa imewanyonga mabingwa hao watetezi baada ya kuonesha hakukuwa na vurugu zozote kama inavyodaiwa na wakali hao wa jangwani.

Mwamuzi Andrew Shamba ripoti yake na ile ya kamishna wa mchezo huo tayari zimetua TFF na zote hazielezi lolote kuhusu vurugu za uwanjani,na hiyo ina maana rufaa ya Yanga haina nguvu yoyote na hata kamati ya ligi haina lolote inaloweza kuamua kuhusu vurugu hizo zinazolalamikiwa na Yanga.

Kwa mujibu wa afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema hata barua ya Yanga iliyopelekwa TFF haina ushahidi wowote unaoonesha kuwa kulikuwa na vurugu uwanjani hali inayolifanya suala hilo kwa Yanga kuwa gumu.

Wambura amesema hata barua yoyote ama rufaa kwenda kwa kamati ya nidhamu ni lazima iwe imekamilika ndipo unapoweza kuitisha kikao cha kamati hiyo lakini kama haina vielelezo vyovyote kamati hiyo haiwezi kukutana.

Yanga Africa wanataka mchezo wao na Mbeya City urudiwe kwakuwa walifanyiwa vurugu kabla ya mchezo huo ambazo ziliwaharibu saikolojia yao na kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.