Wednesday, September 4, 2013

GALATASARY : Manchester United walimtaka Sneijder ofa ikapigwa chini


Manchester United walijaribu bila mafanikio kumsajili kiungo wa Galatasaray Wesley Sneijder katika wakati wa mwisho wa usajili.

Usajili wa kwanza wa David Moyes kama kocha wa United ni kumnasa kiungo Marouane Fellaini.
Moyes alijaribu kuwasajili bila mafanikio Cesc Fabregas, Thiago Alcantara, Leighton Baines, Ander Herrera na Sami Khedira pia ikashindwa dakika za lala salama kumsajili beki wa kulia wa Real Madrid as Fabio Coentrao.

Na sasa imevuja kuwa Moyes pia alimkosa Sneijder ili atue Old Trafford wiki mbili kabla ya usajili kufungwa.
Mkurugenzi wa michezo wa Galatasaray Bulunt Tulun anasema Sneijder alipewa ofa na Manchester United wiki mbili zilizopita lakini ikapigwa chini huku pia akisema kulikuwa na ofa kutoka vilabu vingine kumtaka kiungo huyo na Burak Yilmaz.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.