Boss wa Chelsea Jose Mourinho amekubali kuubeba mzigo wa kipigo cha janacha mabao 2-1 kutoka kwa FC Basel katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Mourinho amesema timu inapopoteza hazungumzi kuhusu wachezaji au mchezaji mmoja mmoja anazungumza kuhusu wajibu wake na akisema anawajibika.
Mshambuliaji mpya Samuel Eto'o alianza kikosi cha kwanza huku Demba Ba akiingia kipindi cha pili na Fernando Torres hakuwepo hata kwenye benchi.
Mourinho amesema hana tatizo na safu yake ya ushambuliaji licha ya kutotupia wavuni.
Anasema wachezaji ni wazuri na wanajaribu kadiri wanavyoweza kila siku na kwenye kila mechi lakini anafahu nyakati za furaha zinakuja.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.