Sunday, September 22, 2013

MOURINHO : Wamekaa kimya

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema baada ya ushindi wa jana watu wamekaa kimya akiwashangaa wanasubiri wafungwe ndio waongee.
Mourinho anasema wakati timu ilipokuwa haipati ushindi yalikuwa yanasemwa maneno mengi wakiponda muelekeo wa timu lakini baada ya matokeo ya jana anashangaa wamekaa kimya wakiiona timu imekaa kileleni ikiongoza ligi.
Anasema kwasasa yupo kwenye kuijenga upya timu hiyo kwaajili ya mafanikio ya baadaye.

Chelsea kwenye mchezo wa jana ikiwa ugenini ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0 yakipachikwa wavuni na Oscar na Mikel Obi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.