Kocha Giovanni Trapattoni amebwaga kibarua chake cha kuinoa Jamhuri ya Ireland kufuatia kichapo kutoka kwa Austria kwenye mchezo wa kuisaka tiketi ya fainali za kombe la dunia.
Chama cha soka cha Ireland kimetangaza kuondoka kwa Trapattoni na msaidizi wake Marco Tardelli baada ya kikao walichofanya nao licha ya kuwa wana mkataba uliotakiwa kumalizika May 2014.
Katika miaka yake mitano akiwa kocha wa Ireland, Trapattoni aliipeleka timu hiyo kwenye fainali za Euro 2012.
Kimahesabu katika michezo ya kusaka tiketi ya fainali za kombe la dunia inaweza ikaivuka Sweden na kukalia nafasi ya pili ya kundi C.
Trapattoni ameshukuru ushirikiano walioupata katika muda wote akiifundisha timu hiyo.
Rekodi ya Trapattoni akiwa na Ireland
- Matches: 64
- Wins: 26
- Draws: 22
- Defeats 16
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.